2 Kings 22:1-2

Yosia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 34; 35:20-27)

1 aYosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. 2 bAkafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.

Copyright information for SwhKC